Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu hao ambao hawaja jisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.
"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.
Amesema kati ya watu waliotajwa ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.
Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao awako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.
Wema Sepetu. |
Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao awako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.
CP Simon Sirro
Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.
Vanessa Mdee |
Tunda (Video za miziki Tz ni maarufu Video Qeen) |
Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"
Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo.