Friday, February 3, 2017

MADAWA YA KULEVYA (Unga) Dar es Salaam,

WAHUSIKA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA (Unga) WAKAMATWE.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja kuhusika na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi , kama alivyoagiza


       




Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu hao ambao hawaja jisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.
"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.
Amesema kati ya watu waliotajwa ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.

Wema Sepetu.

Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao awako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.    

CP Simon Sirro

 Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.

Vanessa Mdee
Tunda (Video za miziki Tz ni maarufu Video Qeen)
Mbali na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.
Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"
Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo.

1 comment:

  1. Kama tunawatuhumu wauza Unga !!!! Nawatumia unga
    Tuwataje wote na wao wawataje wengine
    Mfano haiwezekani kumtaja mmoja nawakati ana mtuwake wakaribu kama mpenzi ama rafiki sana ikawa hausiki atakama nibiashara za siri sana wana mbinu na nguvu ya pesa kumjua ama kuishi na mwalifu atakama ujihusishi ww pia unatakiwa ukajisalimishe nimtazamo wangu maana ndo washatajwa ivo Wasanii 7 waliojisalimisha ndani Police ijumaa ni 4 wawaili wanatafutwa na maasikari 12 watuhumiwa kwakushirikiana na wauza Unga wameshasimamishwa kazi jana jmos tareh 4/2
    Mkuu wa Dar slam Paul Makonda ameagiza wakutane j3. Nahao inwezekana hawawajui maboss wakubwa wanatumika tu yani anaye tumwa mzigo naye anatuma anayepokea ni mwingine nawanao sambaza ni wengine apo ukishikwa ufe mwenyewe Sasa kama hawa walio tajwa ni wausika maana mm naamini hadi wataje kwa majina Wasanii wakubwa ivi na polic kweli uchunguzi wanguvu umeshafanyika ushahidi tu ndo nadhani hawana Watafanya mahojiano nao then labda kama wanapicha za biashara ila ushahidi wapicha mahakamani hauna nguvu sana
    Wakipata tu maelezo wanayo yataka watawaachia
    Na hawa maaskari 12 sidhani kama wanaweza rudishwa kazi maana serkalini kazi ukshapata tuhuma yyte kubwa ivo ikitegemea ishukubwa ivo lazima kwanamna yyote unajua au unahusika au Unatumia Unga
    Mmmh msije mkanijumlisha na mm maana naonekana najua sanaaa
    Nimejulia kwe maMoviez jamani mwayaae.

    ReplyDelete