MAREKANI Tar 20/01/2017,
Raia walihudhuria kuonyesha umoja wao na wengine wakipinga wakati Donald Trump akiapishwa kuwa rais wa Marekani.
Aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama akipunga mkono kusema kwaheri wakati alipoingia katika ndege na kuondoka, huku Donald Trump na mkewe wakirudi katika jengo la Capitol Hill.
Rais Donald Trump kushoto na rais wa zamani Barrack Obama wakiwa na wake zao nyuma yao, wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa taifa.
Jackie Evancho, mshiriki wa shindano la Got Talent ndiye aliyeimba wimbo wa taifa wa Marekani katika sherehe hizo.
Kwa wengine ilikuwa furaha isio kifani na ukumbusho wa ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi uliopita dhidi ya Hillary Clinton.
Lakini maelfu ya waandamani walihudhuria kuonyesha hasira zao walijaribu kufunga njia kuingia katika eneo la Capitol ambapo rais Trump aliapishwa raasmi kuwa rais wa 45 wa Marekani.
No comments:
Post a Comment