Friday, February 3, 2017

MADAWA YA KULEVYA (Unga) Dar es Salaam,

WAHUSIKA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA (Unga) WAKAMATWE.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja kuhusika na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi , kama alivyoagiza


       




Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu hao ambao hawaja jisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.
"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.
Amesema kati ya watu waliotajwa ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.

Wema Sepetu.

Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao awako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.    

CP Simon Sirro

 Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.

Vanessa Mdee
Tunda (Video za miziki Tz ni maarufu Video Qeen)
Mbali na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.
Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"
Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo.

Friday, January 27, 2017

AL-SHABAB SOMALIA

Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.





Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.

Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.

Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."

Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.


Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.

Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.

Sunday, January 22, 2017

CHUO CHA USAFIRISHAJI- NIT

NIT (National Institute of Transportation) Tanzania
Pekee Mabibo mwisho Dar es Salaam.
Nawadau wengine wakitoa Zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri.


Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Prof.Zacharia Mganilwa akimuonesha Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga maeneo mbalimbali ya chuo hicho wakati wa kongamano lililowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma katika chuo hicho katika miaka ya nyuma na waliomaliza mwaka ulioisha wa masomo.



Baadhi wa wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakiwa katika kongamano lililowakutanisha na viongozi wa chuo hicho.


Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.Zacharia Mganilwa akiongea na wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo hicho ambapo alisema dhumuni la kuwakutanisha ni kutoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao ikiwa ni lengo la kuongeza ufaulu na kuwa na wanafunzi bora ambao wanaweza kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi kwa kutumia elimu waliyoipata kutoka chuoni hapo.
Ambapo mgeni mrasmi naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga alisema taasisi yake itaendelea kuonesha nia ya kukisaidia chuo hicho ili kiendelee kukua zaidi na kutoa wahitimu bora katika soko la ajira nchini na afrika kwa ujumla.


Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao wakipewa zawadi kutoka kwa wadau katika sekta ya usafirishaji nchini.


Dkt. John Layaa kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji akitoa mada kuhusu umuhimu wa usafirishaji katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi wakati wa kongamano la 3 la wanafunzi waliowahi kusoma chuoni hapo,  Jijini Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga (Mwenyeshati jeupe)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) na wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao.

TRUMP RAIS.

Saturday, January 21, 2017

MATAJIRI (MABILIONEA) WAKUBWA DUNIANI.


Wanane hawa wanamiliki uchumi wawatu wengi sana mil3,


Bill Gates

Takwimu za shirika hilo, ambazo zimepingwa na baadhi ya wakosoaji, zinatokana na maelezo na habari za kina zilizokusanywa na shirika hilo, na zinaonesha pengo kati ya matajiri na maskini ni kubwa "kuliko ilivyodhaniwa awali".
Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa wakati mkutano mkubwa kuhusu uchumi wa dunia unaanza mjini Davos nchini Uswisi.
Mark Littlewood, wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi, amesema Oxfam inapaswa kuangazia njia ya kusisimua ukuaji wa uchumi   wa dunia badala ya kufanya utafiti huo.
Oxfam imekuwa ikitoa ripoti zinazokaribiana kwa miaka minne iliyopita ambapo mwaka 2016 ilifichua kwamba watu 62 duniani walikuwa na utajiri sawa na wa nusu ya watu maskini zaidi duniani.
Lakini bado hali ni ile ile, kwamba asilimia moja ya watu duniani wanamiliki utajiri sawa na watu hao wengine wote duniani kwa pamoja.

Amancio Ortega


Mabilionea wanane matajiri zaidi duniani ni:
1. Bill Gates (US): mwanzilishi wa Microsoft (utajiri wake $75bn)
2. Amancio Ortega (Spain): mwanzilishi wa Zara na mmiliki wa Inditex (utajiri wake $67bn)
3. Warren Buffett (US): mwenyehisa mkubwa Berkshire Hathaway (utajiri wake $60.8bn)
4. Carlos Slim Helu (Mexico): mmiliki wa Grupo Carso (utajiri wake $50bn)
5. Jeff Bezos (US): mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa Amazon (utajiri wake $45.2bn)
6. Mark Zuckerberg (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Facebook (utajiri wake $44.6bn)
7. Larry Ellison (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Oracle (utajiri wake $43.6bn)
8. Michael Bloomberg (US): mmiliki wa Bloomberg LP (utajiri wake $40bn)

Warren Buffett
Chanzo: Orodha ya mabilionea ya Forbes.