Kundi lililo
na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda nchini Syria Al- Nusra Front
limepinga mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na muungano unaoongozwa
na Marekani kama vita dhidi ya Uislamu na kusema kuwa nchi za Magharibi
na zile za Kiarabu zinazohusika zitalengwa na makundi ya Jihad kote
duniani.
Matamshi
hayo yanatolewa baada ya Marekani kusema kuwa ushirikiano na washirika
wake wa Kiarabu umefanya mashambulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa
Islamic State nchini Syria na Iraq.
Wizara ya
ulinzi nchini Marekani ilisema kuwa ndege za kijeshi zilishambulia mji
wa Raqqa nchini Syria ambao ni ngome ya wanamgambo pamoja na maeneo
yanayodhibitiwa na kundi la Islamic state karibu na mji wa Kikurdi wa
Kobane karibu na mpaka na Uturuki.
No comments:
Post a Comment