Tuesday, September 30, 2014

Dar es Salaam Jeshi la Polisi kanda maalum kuwatawanya wafuasi wa chama cha CHADEMA waliokuwa wakiandamana eneo la Manzese kilimani ili kupinga vikao vya bunge maalum la katiba. eneo hilo walikuwa wamefanikiwa kufanya maandamano wakiimba nyimbo za hamasa kuonyesha kufurahishwa kwao na kutimiza lengo lao ghafla askari polisi walivamia na kuanza kufyatua risasi za moto na mabomu ya machozi kitendo kilichowafanya waandamanaji hao kukimbilia katika makazi ya watu.Picha kutoka sehemu kama hizo husika

Sunday, September 28, 2014

 

AL-NUSRA FRONT  VITA! YATANGAZWA.

Kundi lililo na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda nchini Syria Al- Nusra Front limepinga mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na muungano unaoongozwa na Marekani kama vita dhidi ya Uislamu na kusema kuwa nchi za Magharibi na zile za Kiarabu zinazohusika zitalengwa na makundi ya Jihad kote duniani.

Matamshi hayo yanatolewa baada ya Marekani kusema kuwa ushirikiano na washirika wake wa Kiarabu umefanya mashambulizi zaidi dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
Wizara ya ulinzi nchini Marekani ilisema kuwa ndege za kijeshi zilishambulia mji wa Raqqa nchini Syria ambao ni ngome ya wanamgambo pamoja na maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Islamic state karibu na mji wa Kikurdi wa Kobane karibu na mpaka na Uturuki.

Friday, September 26, 2014

DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada. Na Daniel Makaka, Sengerema
NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza. Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu. Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia. Serikali itaendelea kusaidia kadri iwezavyo si kwamba watapewa fidia bali ni misaada tu. Awali Katibu wa kamati ya maafa wilaya Sengerema Bw. Benard Myatilo akitoa taarifa ya wahanga wa tukio hilo alisema kuwa matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ambapo Septemba 19 majira ya saa nane usiku kaya 40 ziliteketea kwa moto na chanzo cha moto huo ni kulipuka kwa Kibatari ndani ya nyumba na tukio la pili kaya 11 kuezuliwa na mvua ilyoambatana na upepo likiwemo jengo la kanisa Katoliki kisiwani humo. Pia alisema kati ya wahanga hao hakuna mtu aliyejeruhiwa katika matukio hayo licha mali zote zlizokuwemo kuteketea ambapo hadi sasa kaya saba hazina mahali pakuishi huku zilizobaki zikihifadhiwa na baadhi ndugu na jamaa wanaoishi katika kisiwa hicho.